Swali: Je, inajuzu kuswali nyuma ya imamu mwenye kunyoa ndevu zake na anaamrisha watu wanyoe ndevu zao?

Jibu: Huyu haitakikani kuwa imamu wa watu. Inatakiwa kupelekwa suala lake kwa wasimamizi ili wamuondoshe na waweke mwingine. Mwenye kunyoa ndevu zake na anaamrisha wengine wanyoe ndevu zake hastahiki kuwa imamu. Inatakiwa kuondoshwa. Lakini hata hivyo lau mtu ataswali nyuma yake, inasihi Swalah yake. Ni mfanya madhambi. Swalah nyuma ya mfanya madhambi inasihi. Kuswali nyuma ya mfanya madhambi ambaye sio kafiri, inasihi. Lakini hastahiki kufanywa kuwa imamu. Mwenye kujulikana kuwa ananyoa ndevu zake, hatakiwi kufanywa kuwa imamu. Lipelekwe suala lake kwa wasimamizi mpaka aweze kubadilishwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=12822
  • Imechapishwa: 20/11/2014