Swali: Vipi kuhusu imamu anawaswalisha watu na wala hafungi mikono katika Swalah yake?

Jibu: Jambo hili ni limechukizwa [Makruuh]. Swalah yake ni sahihi, lakini ameacha Sunnah. Sunnah ni kufunga mikono namna hii: kuweka mkono wa kulia juu ya wa kushoto juu ya kifua. Namna hii ndivyo alivyokuwa akifanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaposwali kwa kusimama. Anaweka mkono wa kulia juu ya wa kushoto juu ya kifua. Lau ataachia, hili ni jambo limechukizwa lakini Swalah yake ni sahihi. Hata hivyo atakuwa ameacha jambo bora ambalo ni Sunnah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=12822
  • Imechapishwa: 20/11/2014