Swali: Vijiji vina haja kubwa ya walinganizi. Tulisafiri katika kijiji kimoja. Hakukuweko mlinganizi hata mmoja.

al-Albaaniy: Ndio. Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu!

Swali: Kila siku ya ijumaa wanajiwa na mmoja katika Jamaa´at-ut-Tabliygh na unajua kile wanachozungumza.

 al-Albaaniy: Ndio. Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu!

Swali: Hivi punde tulikuwa ´Aqabah. Wanasema kuwa wametupwa na kwamba ´Aqabah wanahitajia wanalinganizi. Ni wenye kukubali zaidi kuliko watu wa ´Ammaan.

Jibu: Hapana shaka kwamba safari hizi zinanufaisha sana. Lakini yule anayetaka kusafiri ni lazima awe ima mwanachuoni au mwanafunzi mwenye nguvu kabisa. Kwa sababu mtu huyu atakumbana na kuulizwa maswali ambayo hakujiandaa nayo na hivyo ajibu pasi na elimu. Matokeo yake faida yake inakuwa khasara. Kwa hivyo safiri hizi ni lazima, lakini sio kwa mtindo wa  Jamaa´at-ut-Tabliygh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (903)
  • Imechapishwa: 03/01/2021