Mabaki ya chakula kati ya meno na kucha na wudhuu´

Swali: Kule kubaki kwa chakula kati ya meno na chini ya kucha kunaathiri wudhuu´?

Jibu: Hakuchengui wudhuu´ kwa kubaki kwake. Lakini haitakiwi kwa mtu kubakiza chakula kati ya meno yake. Anatakiwa kukiondosha. Chakula kinachobaki chini ya kucha kinakuwa kichache na hivyo anatakiwa kukiondosha. Haifai akaacha kucha zikawa refu wala kuziacha zaidi ya nyusiku arobaini. Kucha, masharubu, nywele za sehemu ya siri na nywele za kwapani haziachwi zaidi ya nyusiku arobaini.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (18)
  • Imechapishwa: 03/01/2021