Mtu anaweza kulipa siku sita za Shawwal baada ya kumalizika mwezi wa Shawwaal?

Swali: Kuna mwanamke ilimjilia hedhi ndani ya Ramadhaan kisha akalipa siku hizo kisha akaifuatishia siku sita za Shawwaal. Je, anapata ujira?

Ibn Baaz: Amefunga ndani ya mwezi wa Shawwaal?

Muulizaji: Hapana. Mwezi wa Shawwaal ulimalizika na hakuwahi kufunga zile siku sita.

Jibu: Shawwaal ikimalizika hakuna tena funga. Wakati wake umekwishapita. Lakini afunge… afunge siku tatu za kila mwezi au afunge jumatatu na alkhamisi kila mwezi. Zote hizo ni kheri. Fadhilah za Allaah ni pana.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23342/حكم-قضاء-ست-شوال-بعد-انتهاء-شوال
  • Imechapishwa: 03/05/2022