Mtu akizowea swalah ya Sunnah inakuwa wajibu juu yake?

Swali: Je, swalah zilizopendekezwa zinakuwa wajibu endapo mtu atajizoweza nazo?

Jibu: Hapana, haziwi wajibu. Swalah iliyopendekezwa siku zote inakuwa iliyopendekezwa. Kamwe haiwi wajibu. Lakini kuhusu hajj na ´umrah mtu akishaingia ndani ya Ihraam basi zinamuwajibikia. Amesema (Ta´ala):

وَأَتِمُّوا الْحَجَّ وَالْعُمْرَةَ لِلَّـهِ

“Timizeni Hajj na ‘Umrah kwa ajili ya Allaah. “[1]

Hili ni kitu maalum katika hajj na ´umrah. Mtu akishaingia ndani ya Ihraam basi kutamlazimu azikamilishe. Kuhusu mengineyo – kama mfano wa swalah, swawm, swadaqah na mengineyo – ni mambo yaliyopendekezwa ambayo hubaki kuwa yamependekezwa.

Endapo mtu ataanza kuswali inafaa kwake kuikata. Endapo mtu ataanza kufunga swawm iliyopendekezwa inafaa kwake kuikata. Lakini bora kwake ni yeye kuikamilisha. Endapo atatoa mali ili aende kuitoa swadaqah inafaa kwake kurejea kabla hajamfikishia yule masikini. Lakini bora ni yeye kutorejea katika swadaqah.

Kinacholengwa ni kwamba ´ibaadah zote zilizopendekezwa zinabaki juu ya hali yake ya mapendekezo mpaka atakapozimaliza. Isipokuwa hajj na ´umrah. Akizianza basi zinamlazimu mpaka atakapozikamilisha.

[1] 02:196

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/430)
  • Imechapishwa: 18/11/2021