Mtu anapata dhambi kwa kuacha ´ibaadah za Sunnah alizokuwa akifanya?

Swali: Je, mtu anapata dhambi kwa sababu ya kuacha baadhi ya ´ibaadah zilizopendekezwa ambazo alikuwa ni mwenye kudumu katika kuzitekeleza? Kwa sababu kwa mfano mimi wakati nilipokuwa mjamzito niliacha kufunga jumatatu na alkhamisi.

Jibu: ´Ibaadah zilizopendekezwa zote analipwa thawabu mwenye nazo na wala hapati dhambi yule mwenye kuziacha. Mfano wake ni kufunga jumatatu na alkhamisi, kufunga siku tatu kila mwezi, Sunnah ya Dhuhaa na Witr. Lakini imesuniwa kwa muumini kudhibiti na kuchunga zile Sunnah zilizokokotezwa. Kwa sababu ndani yake kuna ujira mkuu na thawabu nyingi. Jengine ni kuwa ´ibaadah zilizopendekezwa zinakamilisha yale mapungufu ya faradhi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/431)
  • Imechapishwa: 18/11/2021