Swali: Ni ipi hukumu ya ambaye imempita swalah ya Maghrib na wala hakukumbuka isipokuwa wakati kulipokimiwa swalah ya ´Ishaa?

Jibu: Aswali pamoja nao swalah iliyopendekezwa. Kisha wakitoa salamu ataswali Maghrib kisha ´Ishaa. Hili ndio salama zaidi.

Yapo maoni mengine ya wanazuoni. Yanasema kwamba ataswali pamoja nao ´Ishaa kisha wanaposimama katika Rak´ah ya nne ataketi chini. Atasubiri mpaka pale imamu anatoa salamu na yeye atatoa salamu pamoja naye.

Akiswali ´Ishaa kwanza kisha ndio akaswali Maghrib basi ni mwenye kupewa udhuru. Salama zaidi ni yeye kuswali Maghrib pamoja nao. Kisha wakitoa salamu ataswali Maghrib halafu ataswali ´Ishaa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (23)
  • Imechapishwa: 19/11/2021