Njia salama zaidi kwa msafiri anayeswali ´Ishaa nyuma ya imamu anayeswali Maghrib

Swali: Je, inafaa kwa msafiri kuswali swalah ya ´Ishaa kwa kufupisha pamoja na mkusanyiko unaoswali Maghrib kwa njia ya kwamba ataketi chini baada ya Rak´ah mbili mpaka pale atapotoa salamu pamoja naye?

Jibu: Haya ni maoni ya baadhi ya wanazuoni. Maoni ya pili ni kwamba haifai kwake kufanya hivo kwa sababu swalah ni zenye kutofautiana. Moja ni swalah ya Rak´ah tatu na nyingine ni swalah ya Rak´ah nne. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika si venginevyo imamu amewekwa ili afuatwe. Hivyo msitofautiane naye.”

Kwa hiyo aswali pamoja nao swalah iliyopendekezwa. Wakitoa salamu ndipo ataswali ´Ishaa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (23)
  • Imechapishwa: 19/11/2021