Mtoto kuzuia maovu kwa mkono pindi baba hayuko nyumbani

Swali: Je, inafaa kwa mtoto wa kiume mkubwa kuzuia maovu kwa mkono pindi baba yake hayuko nyumbani?

Jibu: Baba yake akimpa kazi ya kuangalia nyumba anapokuwa hayuko, atasimama nafasi yake katika kuzuia maovu kwa mkono. Kwa sababu amempa kazi. Hivyo anatakiwa kukemea kwa mkono. Kama hakumpa kazi hiyo, atazuia kwa kuongea na si kwa mkono.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (04)
  • Imechapishwa: 15/02/2024