Fanya jimaa kisha ufanye Tayammum

Swali: Je, mtu amwingilie mke wake asipopata maji?

Ibn Baaz: Ina maana yuko nchi kavu?

Mwanafunzi: Maji hayakuwepo. Je, inafaa kwake kumjamii mke wake?

Ibn Baaz: Ina maana yuko nchi kavu na hana maji?

Mwanafunzi: Nchi kavu au mahali kokote.

Swali: Amjamii mke wake na afanye Tayammum ikiwa hana maji. Ni kama jangwani nchi kavu na asiwe na maji.

Swali: Kwa hiyo Tayammum inatosheleza kutokana na kuoga?

Jibu: Tayammum inatosha.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23574/هل-يجامع-اهله-من-لا-يجد-الماء-ويكفيه-التيمم
  • Imechapishwa: 15/02/2024