Mtoto kusimama kumbusu mzazi aliyeingia

Swali: Kila anapoingia baba yangu humsimamia na kumbusu kichwa chake.

Jibu: Jambo ni lenye wasaa. Hadiyth ya Faatwimah inasema kwamba kila pale ambapo anaingia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipo husimama kwa ajili yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kinyume chake. Hivo ndivo walivyopokea jopo la wanazuoni kwa cheni ya wapokezi Swahiyh akiwemo Abu Daawuud. Haafidhw na ´Allaamah Ibn Muflih ameyataja hayo katika ”Kitaab-ul-Aadaab” katika yale yanayompasa mwana juu ya baba yake. Kwa hiyo hapana vibaya kufanya hivo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24257/حكم-القيام-للوالد-وتقبيل-راسه
  • Imechapishwa: 20/09/2024