Swali: Msemo:

السلام على من اتبع الهدى

“Amani iwe juu ya yule mwenye kufuata uongofu.”

ni maalum kwa…

Jibu: Makafiri tu.

Swali: Inafaa kumsalimia hivo muislamu?

Jibu: Hapana, haijuzu. Muislamu anasalimiwa:

السلام عليكم ورحمة الله وبركاته

“Amani, rehema na baraka za Allaah ziwe juu yako.”

 Lakini kafiri ndiye anaambiwa:

السلام على من اتبع الهدى

“Amani iwe juu ya yule mwenye kufuata uongofu.”

au:

السلام على من اتبع الحق

“Amani iwe juu ya yule mwenye kufuata haki.”

Kwa sababu haifai kuanza kuwasalimia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24254/لمن-تقال-السلام-على-من-اتبع-الهدى
  • Imechapishwa: 20/09/2024