Mtawala hana haki ya kusamehe adhabu ya Allaah

Swali: Vipi ikiwa mtawala ataona kutosimamisha adhabu ya Kishari´ah?

Jibu: Hapana, haijuzu. Si kwa mtawala wala mwingine. Manufaa yanapatikana kwa kusimamisha adhabu za Kishari´ah. Haijuzu kwa mfalme, mtawala wa jamhuri wala viongozi wengine kuacha kusimamisha adhabu za Kishari´ah wakiwa ni waislamu. Adhabu zinatakiwa kusimamisha ikiwa ni adhabu zilizowekwa na Allaah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22387/هل-يجوز-للملك-او-الرىيس-ان-لا-يقيم-الحد
  • Imechapishwa: 25/02/2023