Swali: Vipi kuoanisha kati ya mwenye kuona maovu akayakemea kwa njia ya kulipiza kisasi kwa ajili ya Allaah au ayakemee kwa hekima, ulaini na maneno mazuri?

Jibu: Ayakemee kwa hekima. Huku ni katika kukasirika kwa ajili ya Allaah:

ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ وَجَادِلْهُم بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ

“Lingania katika njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mazuri na jadiliana nao kwa ambayo ni mazuri zaidi.”[1]

Asinyamaze. Lakini ikiwa haki yake ndio imekiukwa ni sawa akasamehe na kunyamaza.

[1] 16:125

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22384/كيف-يجمع-بين-الرفق-وبين-الانتقام-لله-تعالى
  • Imechapishwa: 25/02/2023