Mswaliji kujiepusha na kuswali na nguo inayomshughulisha

Swali: Vipi kule kumpa kwake Abu Jahm[1] licha ya kwamba ilimshughulisha?

Jibu: Kunafahamisha kuwa jambo lake ni lenye wasaa na kwamba yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alichukia kuivaa, kwa sababu jambo lake ni muhimu zaidi kuliko jambo la fulani. Sio dalili ya kwamba ni haramu. Hata hivyo mtu ameamrishwa kujiepusha na jambo hili ambalo linamshughulisha.

[1] Aliswali (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwenye Khamiyswah iliyo na mifumo na akatazama mifumo yake. Alipomaliza akasema:

“Ipelekeni kanzu hii kwa Abu Jahm na mniletee Anbajaaniyah ya Abu Jahm. Inanishughulisha kutokamana na swalah yangu.” (al-Bukhaariy, Muslim na Maalik. Imetajwa katika ”al-Irwaa’”” (376). )

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24079/%D9%84%D9%85%D8%A7%D8%B0%D8%A7-%D8%A7%D9%87%D8%AF%D9%89-%D8%A7%D9%84%D9%86%D8%A8%D9%8A-%EF%B7%BA-%D8%A7%D9%84%D8%AE%D9%85%D9%8A%D8%B5%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D8%AA%D9%8A-%D8%A7%D8%B4%D8%BA%D9%84%D8%AA%D9%87
  • Imechapishwa: 25/08/2024