Swali: Mtu anaweza kusema kuwa kuharamishwa kuvaa nguo inayovuka vifundo vya miguu sababu yake ni kiburi?

Jibu: Ni njia inayopelekea huko. Ni kipi kilichomfanya akaburuza nguo kama sio kiburi? Hakuna kingine isichokuwa kiburi.

Swali: Ikiwa mshonaji ndiye kafanya hivo?

Jibu: Aibadilishe na amwamrisha aipandishe, mke wake au ndugu yake aipandishe. Hakuna kilichompelekea kufanya hivo isipokuwa kiburi na kuchukulia wepesi amri ya Allaah na kutojali. Isitoshe huyu  amefungua mlango wa isbaal na majanga. Baadhi ya watu hawajali. Hawajali hata kama kitu kinachukiza. Kwa mtazamo wao wanaona kinachochukiza ni sawa tu. Matokeo yake wanakifanya na hawajali.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24084/هل-تحريم-الاسبال-مقيد-بالتكبر
  • Imechapishwa: 25/08/2024