Msimamo wa kufanana kati ya Raafidhwah na manaswara juu ya Mitume

Manaswara wanadai kwamba wanafunzi wa ´Iysaa ni bora kuliko Ibraahiym, Muusa na Mitume na Manabii wengine wote. Wanasema kuwa Allaah alizungumza nao moja kwa moja kwa vile wanasema kuwa ´Iysaa ndiye Allaah na mwana Wake.

Raafidhwah wanadai kwamba wale maimamu kumi na mbili ni bora kuliko wale Maswahabah wa mwanzo katika Muhaajiruun na Answaar. Wale waliochupa mipaka katika wao wanasema kuwa ni wabora zaidi kuliko Mitume kwa sababu wanaamini kuwa maimamu ni waungu, kama wanavyoamini manaswara juu ya ´Iysaa.

Manaswara wanasema kuwa dini imesalimishwa kwa makasisi na watawa. Halali ni kile walichokihalalisha na haramu ni kile walichokiharamisha na dini ni kile walichokiweka wao katika Shari´ah.

Raafidhwa pia wanasema kuwa dini imesalimishwa kwa maimamu. Halali ni kile walichokihalalisha na haramu ni kile walichokiharamisha na dini ni kile walichokiweka wao katika Shari´ah.

Ama kuhusu wale Shiy´ah waliopindukia, kama mfano wa Ismaa´iyliyyah wasemao kuwa al-Haakim na maimamu wao wengine ndio waungu, wanasema kuwa Muhammad bin Ismaa´iyl alifuta Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wana maoni mengine ambayo yana uchupaji mipaka wa Raafidhwah. Watu hawa ni wenye shari zaidi kuliko mayahudi, manaswara na washirkina wakubwa zaidi. Wanajinasibisha kwa Shiy´ah na kujidhihirisha kwa madhehebu yao.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islâm Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Minhaaj-us-Sunnah an-Nabawiyyah (1/481-482)
  • Imechapishwa: 25/12/2018