3- Vovyote atavyozidiwa na maradhi haifai kwake akatamani kifo. Kutokana na Hadiyth ya Umm-ul-Fadhw (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye amesimulia:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliingia nyumbani kwao na ´Abbaas, ami yake Mtume wa Allaah, anaumwa. ´Abbaas akatamani kifo. Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ee ami! Usitamani kifo. Ukiwa ni mwenye kufanya vyema, basi kuchelewa kwako utazidisha wema juu ya wema na hilo ni bora kwako na ukiwa ni mwenye kufanya vibaya, basi kuchelewa kwako utaweza kutubia na hilo ni bora kwako. Hivyo usitamani kifo.”

Ameipokea Ahmad (02/339), Abu Ya´laa (7076), al-Haakim (01/339) ambaye amesema: “Ni Swahiyh juu ya masharti ya al-Bukhaariy na Muslim” na adh-Dhahabiy akaafikiana naye. Uhalisia wa mambo ni kwamba iko juu ya masharti ya al-Bukhaariy peke yake.

al-Bukhaariy na Mulim, al-Bayhaqiy (03/377) na wengineo wamepokea Hadiyth mfano wake kupitia kwa Anas ambaye kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ikiwa hana budi, basi aseme: “Ee Allaah! Nibakize kuwa hai ikiwa uhai ni kheri kwangu na nifishe ikiwa kufa ni kheri kwangu.”

Imepokelewa vilevile katika “al-Irwaa´” (683).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 04
  • Imechapishwa: 25/12/2018