Swali: Je, jirani ambaye ni mzushi anazo haki za majirani muislamu?

Jibu: Muda wa kuwa bado ni muislamu anazo haki kama waislamu wengine. Kwa msemo mwingine ikiwa Bid´ah zake hazimtoi katika Uislamu anazo haki za waislamu wengine. Lakini jirani yake anatakiwa kutaamiliana naye tofauti na anavyotaamiliana na wanaofuata Sunnah na wasiokuwa wazushi. Mzushi analinganiwa kuacha Bid´ah yake na kushikamana na Sunnah. Akiendelea juu ya Bid´ah basi jirani yake atamkata. Hatakiwi kumsalimia, kumzungumzisha na wala asimpe chochote. Pengine akatubu na kujirejea. Ikiwa ni katika walinganizi wa Bid´ah na wenye kuzieneza, basi atahadharishwe kwa kumtaja jina lake na utu wake ili asiidhuru jamii. Mzushi Bid´ah yake ni kama maradhi. Huzieneza na zikawaathiri watu mmojammoja katika wavulana na wasichana. Anapokuja haanzi moja kwa moja kwa kueneza Bid´ah zake. Anapokuja huanza kwa kueneza kati yao Sunnah ili wampende. Kisha baada ya hapo ndio huanza kueneza Bid´ah zake na watu wakadanganyika naye. Matokeo yake wakakubali zile Bid´ah anazoeneza. Kwa sababu hapo kitambo wamekwishatambua kuwa mtu huyu anazungumza na kuwalingania watu katika Sunnah.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah (08)
  • Imechapishwa: 17/12/2023