341 – Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

خير مساجد النساءِ قَعْرُ بيتِهِن

“Bora ya misikiti ya wanawake ni ile sehemu ya ndani kabisa katika majumba yao.”[1]

Ameipokea Ahmad na at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr”. Kwenye cheni yake ya wapokezi yuko Ibn Lahiy´ah. Ibn Khuzaymah pia ameipokea katika ”as-Swahiyh” yake na al-Haakim kupitia kwa Darraaj Abus-Samh, kutoka kwa as-Saa-ib, mtumwa wa Umm Salamah aliyemwacha huru. Ibn Khuzaymah amesema:

“Sijui juu ya kusifiwa wala kujeruhiwa kwa as-Saa-ib, mtumwa wa Umm Salamah aliyemwacha huru.”

al-Haakim amesema:

“Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh.”

[1] Nzuri kupitia zingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/259)
  • Imechapishwa: 17/12/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy