Ahl-us-Sunnah wanashuhudia ya kuwa waumini watamuona Mola wao (Tabaarak wa Ta´ala) kwa macho yao na watamtazama, kutokana na zilivyopokelewa khabari Swahiyh kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Hakika nyinyi mtamuona Mola wenu kama mnavyouona mwezi usiku wa mwezi mng´aro.”[1]

Ufananishaji uliyotajwa hapo juu ni kuhusiana na kuona na si kile kitachoonwa. Hadiyth kuhusu Kuonekana na cheni zake za wapokezi zimekaguliwa katika kitabu ”al-Intiswaar”.

[1] al-Bukhaariy (573) na Muslim (296).

  • Mhusika: Imaam Abu ´Uthmaan Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy (afk. 449)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 263-26
  • Imechapishwa: 18/12/2023