Ahl-us-Sunnah wanashuhudia ya kwamba Pepo na Moto vimekwishaumbwa na kwamba ni vyenye kubaki na kamwe havitokwisha, kwamba wakazi wa Peponi kamwe hawatotoka humo na pia wakazi wa Motoni, ambao ndio wakazi wake kikweli na ambao wameumbiwa nao, kamwe hawatotoka humo. Kifo kitaletwa na kuchinjwa kwenye ukuta kati ya Pepo na Moto. Siku hiyo ataita mwitaji:

”Enyi watu wa Peponi! Dumuni milele na wala hakuna kifo tena! Enyi wakazi wa Motoni! Dumuni milele na wala hakuna kifo tena!”[1]

Hivo ndivo zimesihi khabari Swahiyh kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] Muslim (2849).

  • Mhusika: Imaam Abu ´Uthmaan Ismaa´iyl bin ´Abdir-Rahmaan as-Swaabuuniy (afk. 449)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 264
  • Imechapishwa: 18/12/2023