Epukeni kuingia msikitini na nguo zenye picha

Swali: Ni ipi hukumu ya swalah ya ambaye kwenye nguo zake kuna picha? Unamnasihi nini ambaye anaingia msikitini na nguo zenye picha?

Jibu: Nasaha zangu ni kwamba haijuzu kwake kuvaa nguo zenye picha na akaingia nazo msikitini. Bali ni lazima kwake kuitakasa nafsi yake na misikiti kutokana na kuvaa nguo zilizo na picha zenye viumbe wenye roho. Ni mamoja viumbe hao ni wanadamu au wanyama. Hata hivyo siwezi kuhukumu kuwa swalah yake ni batili. Lakini ni mwenye kupata madhambi na amefanya kosa. Ni lazima kujiepusha na jambo hilo.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah (08)
  • Imechapishwa: 17/12/2023