Msimamo kwa jamii yenye kwenda kinyume na ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah

Swali: Mwanafunzi na mlinganizi wafanye nini wanapokuwa katika jamii ilio na fikira na madhehebu yenye kwenda kinyume na ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah?

Jibu: Ni wajibu kwake kujua ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Ajifunze nayo na aijue kwanza. Ashikamane nayo popote pale. Ashikamane nayo hata kama watu wa mji wake wanaenda kinyume naye. Awapuuze na ashikamane nayo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (26) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir%20ayat-03-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 21/06/2020