Swali: Mmoja katika wale watu waliokuja nyuma akifasiri Aayah ya Qur-aan kwa njia ya kushangaza na ya kukinaisha. Je, tuirudishe tafsiri hiyo kwa kuzingatia kwamba ni tafsiri inayoenda kinyume na tafsiri ya Salaf?

Jibu: Wale waliokuja nyuma wakifasiri Aayah ya Qur-aan kwa tafsiri ambayo haikuzungumziwa na wa mwanzo wale waliotangulia na wakati huohuo haikwenda kinyume na tafsiri yao, basi itachukuliwa. Kwa mfano wamefasiri Aayah nyingi za kilimwengu ambazo imekuja kubainika baada ya miaka kwa vile tafsiri yazo ilikuwa si yenye kutambulika hapo kabla. Lakini ikiwa zinakwenda kinyume na tafsiri ya Salaf, kwa mfano tafsiri ya kuwa juu (الإستواء) ya ´Arshiy kwamba ni kutawala (الإستيلاء) juu ya ´Arshiy, tafsiri hii ni lazima kurudishwa nyuma na haifai kuikubali.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (25 B) Dakika: 24:25
  • Imechapishwa: 22/09/2021