Swali: Mmoja katika ndugu amesoma katika kijitabu kilichokuwa kinatawanywa ya kwamba mwisho mwa zama fitina zitakuwa nyingi ambapo mtu ima atakimbilia Shaam au Yemen. Je, upi sahihi wa Hadiyth hii?

Jibu: Zimepokelewa Hadiyth tele kabisa, au zinakaribia kuwa Hadiyth tele, juu ya fitina mwishoni mwa zama. Hata hivyo sijui Hadiyth yoyote Swahiyh inayosema kukimbilia Shaam au Yemen. Kuzikimbia fitina kunakuwa kwa kuondoka katika miji. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kunakaribia bora ya mali ya mtu itakuwa ni wanyamahoa anaowaongoza vilele vya milima na mabonde kwa ajili ya kuzikimbia fitina.”

Lakini yule anayeweza kubaki, akasubiri na akawalingania watu katika mambo ya kheri basi itakuwa ndio wajibu na jambo lenye manufaa zaidi kwake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (17 B) Dakika: 23:32
  • Imechapishwa: 22/09/2021