Hakika tumepewa mtihahi wa wajinga katika watu ambao wanafikiri kuwa baadhi ya wale waliokuja nyuma ambao wameingia zaidi kwa undani katika mambo ya kielimu kuwa ni wajuzi zaidi kuliko wale waliotangulia. Miongoni mwao wako wanaofikiri kuwa baadhi ya watu waliokuja nyuma ni wajuzi zaidi kuliko Maswahabah wote na waliokuja baada yao kwa sababu ya ubainifu na maneno yao mengi. Wengine wanaona kuwa ni wajuzi zaidi kuliko wale wanazuoni wanaotambulika na wanaofuatwa, kitu ambacho kinapelekea katika kile cha kabla yake. Kwa sababu wanazuoni hawa wanaotambulika na wanaofuatwa wamezungumza sana kuliko walivofanya wale wa kabla yao. Kwa hivo ikiwa wale waliokuja baada yao ni wajuzi kuliko wao kwa sababu tu eti wamezungumza sana, basi wana haki zaidi ya kuwa wajuzi zaidi kuliko wale waliozungumza machache, kama mfano wa ath-Thawriy, al-Layth, Ibn-ul-Mubaarak na wale watu walioko katika ngazi yao na pia wanafunzi wa Maswahabah na Maswahabah wenyewe – kwani wote hawa wana maneno machache kuliko wale waliokuja baada yao. Fikira kama hiyo ni utovu wa adabu mkubwa juu ya Salaf na kuwajengea dhana mbaya na kuwanasibishia ujinga na uchache wa elimu. Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema kweli pale aliposema juu ya Maswahabah:

“Nyoyo zao zilikuwa na uchaji zaidi, elimu yao ilikuwa yenye kubobea zaidi na wachache wa kujikakama.”[1]

Maneno kama hayo yamepokelewa kutoka kwa Ibn ´Umar pia. Hapa kuna maashirio kwamba zile karne za wale wataokuja baada yao watakuwa na elimu chache, kujikakama kwa wingi. Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema tena:

“Hakika nyinyi mnaishi katika kipindi ambapo kuna wanazuoni wengi na wahubiri ni wachache. Lakini baada yenu kutakuja kipindi ambapo wanazuoni watakuwa wachache na wahubiri watakuwa wengi.”[2]

Yule ambaye atakuwa na elimu nyingi lakini anazungumza machache ni mwenye kusifiwa, na yule ambaye atakuwa na elimu chache lakini anazungumza mengi ni mwenye kusemwa vibaya.

[1]Jaami´ Bayaan-il-´Ilm wa Fadhwlih, uk. 419, na Mishkaat-ul-Maswaabiyh (193).

[2]Abu Khaythamah katika ”al-´Ilm” (109), at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam as-Swaghiyr” (8566) na al-Bukhaariy katika ”al-Adab al-Mufrad” (789).

  • Mhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn bin Rajab al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Fadhwl ´Ilm-is-Salaf ´alaa ´Ilm-il-Khalaf, uk. 65-66
  • Imechapishwa: 22/09/2021