Msemo unaosema Qur-aan imeteremshwa kwa mkupo mmoja kutoka Bayt-ul-´Izzah

Swali: Je, Qur-aan Tukufu imeshuka kwa jumla wakati mmoja kutoka Bayt-ul-´Izzah kwenye mbingu ya dunia usiku wa cheo kitukufu (Laylat-ul-Qadr) na halafu baada ya hapo ikashuka kidogo kidogo kwa kutegemea na hali ya mambo?

Jibu: Haya yamepokelewa lakini hata hivyo sio sahihi. Sio sahihi. Qur-aan imeanza kuteremshwa katika Laylat-ul-Qadr. Kisha baada ya hapo ikaendelea kushuka kidogo kidogo kwa kiasi cha hali ya mambo ilivokuwa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haikushushwa jumla kwa wakati mmoja. Athar hii haikuthibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Shaykh Muhammad bin Ibraahiym (Rahimahu Allaah) ameandika kijitabu juu ya hili ambapo amemraddi as-Suyuutwiy alosema hivi na akabatilisha msemo huu. Kijitabu hicho amekiita “al-Jawaab-ul-Qaadhwih al-Mustaqiym fiy Kayfiyyat-un-Nuzuul-il-Qur-aan al-Kariym”. Kimechapishwa kipekee na kimechapishwa vilevile kikiwa pamoja na fataawa zake Shaykh (Rahimahu Allaah).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (14) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-10-15.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020