Msemo kwamba hakuna hayaa katika dini

Swali: Msemo unaosema:

“Hakuna hayaa katika dini.”

ni sahihi?

Jibu: Sijui msingi wake. Msemo huo umechukuliwa kutoka katika maneno ya Umm Sulaym alisema maneno yenye maana kama:

“Ee Mtume wa Allaah! Hakika Allaah hastahi juu ya haki.”

Msemo huo umechukuliwa kutoka hapa. Akauliza:

“Ee Mtume wa Allaah! Je, ni lazima kwa mwanamke kuoga josho ya janaba anapoota?”

Akauliza na kwamba si mwenye kuona hayaa kwa sababu anauliza jambo muhimu. Akamjibu:

“Ndio. Akiona manii.”

Isitoshe Allaah (Ta´ala) amesema:

وَاللَّهُ لَا يَسْتَحْيِي مِنَ الْحَقِّ

“ Allaah hastahi haki.”[1]

[1] 33:53

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22688/ما-صحة-قول-لا-حياء-في-الدين
  • Imechapishwa: 18/07/2023