Aliyewahi Rak´ah ya moja amepata fadhilah za Takbiyrat-ul-Ihraam?

Swali: Ambaye amewahi Rak´ah moja amewahi fadhilah za Takbiyrat-ul-Ihraam?

Jibu: Hapana, maoni ya sawa ni kwamba hakuwahi fadhilah zake isipokuwa kwa kuileta.

Swali: Ikiwa alikuwa anaswali swalah ya mamkuzi ya msikiti…

Jibu: Aikate.

Swali: … ilihali anajua kuwa atakosa Takbiyrat-ul-Ihraam?

Jibu: Kukikimiwa swalah basi aikate swalah ya mamkuzi ya msikiti na alete Takbiyrat-ul-Ihraam na imamu. Afanye hivo hata kama amekwishaswali Rak´ah moja. Isipokuwa kama yuko katika Rak´ah ya mwisho na ameshafika katika Rukuu´ ya pili, katika hali hiyo aikamilishe kwa sababu kilichobaki ni kifupi na hivyo atawahi [fadhilah zake] – Allaah akitaka.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22683/ما-الذي-يدرك-به-فضل-تكبيرة-الاحرام
  • Imechapishwa: 18/07/2023