30. Imani iliyokusanyika kwa mtu

131 – Wakiy´ ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Abu Ishaaq[1], kutoka kwa Silah, kutoka kwa ´Ammaar (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye amesema:

”Mambo matatu – yule mwenye kuyakusanya ameikusanya imani; kuifanyia inswafu nafsi yako, kuwatolea salamu viumbe na kujitolea wakati wa hali ngumu.”[2]

132 – Wakiy´ ametuhadithia, kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Abu Ishaaq[3], kutoka kwa Silah, kutoka kwa ´Ammaar (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye amesema kuhusu maneno Yake:

إِنَّهُمْ لَا أَيْمَانَ لَهُمْ

”… hakika viapo vyao havina maana… ”[4]

”Bi maana hawana ahadi yoyote.”

133 – Jariyr ametuhadithia, kutoka kwa Mansuur, kutoka kwa Ibraahiym[5], ambaye alikuwa akisema:

”Hatoingia Motoni mtu ambaye moyoni mwake mna imani sawa na chembe ya haradali[6].”[7]

134 – Zayd bin al-Hubaab ametuhadithia, kutoka kwa as-Sa´q bin Hazn al-Bakriy[8], ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Kishikilio imara zaidi cha Uislamu ni kupenda kwa ajili ya Allaah na kuchukia kwa ajili ya Allaah.”

135 – Abu Usaamah ametuhadithia, kutoka kwa Jariyr bin Haazim: ´Iysaa bin Haazim amenihadithia: ´Adiy bin ´Adiy[9] amenihadithia: ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz aliniandikia:

”Imani ni faradhi, Shari´ah, mipaka na mambo yanayopendeza. Yule mwenye kuyakamilisha, basi ameikamilisha imani. Na yule ambaye hakuyakamilisha, basi hakuikamilisha imani. Nikiishi muda mrefu, basi nitakubainishieni ili mpate kuyatendea kazi. Na endapo nitakufa kabla ya hapo, basi si mwenye kutamani urafiki wenu.”[10]

[1] as-Sabiy´iy. Tayari hivi sasa umekwishajua hali yake hivi punde kidogo.

[2] Swahiyh. Hivo ndivo ameipokea al-Bukhaariy kwa cheni ya wapokez pungufu na Ibn Abiy Shaybah katika ”al-Iymaan” na Ibn Hibbaan katika ”Rawdhwat-ul-´Uqalaa´” kwa cheni ya wapokezi ilioungana.

[3] as-Sabiy´iy. Tayari hivi sasa umekwishajua hali yake hivi punde kidogo.

[4]  9:12

[5] Ibraahiym bin Yaziyd an-Nakha´iy.

[6] Bi maana Moto wa kudumu milele usiomalizika. Tazama (139) na (33).

[7] Cheni ya wapokezi kwenda mpaka kwa Ibraahiym ni Swahiyh.

[8] Alikuwa ni mmoja katika wanafunzi wa wanafunzi wa Maswahabah na alikuwa ni mwaminifu. Kuna wapokezi wengi wanakosekana mfululizo katika cheni ya wapokezi. at-Twabaraaniy ameipokea kwa cheni ya wapokezi ilioungana kupitia kwa as-Sa´d, kutoka kwa ´Aqiyl al-Ja´diy, kutoka kwa Abu Ishaaq al-Hamadaaniy, kutoka kwa Suwayd bin Ghaflah, kutoka kwa ´Abdullaah bin Mas´uud, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). al-Haakim ameisahihisha tofauti na adh-Dhahabiy. Hata hivyo at-Twabaraniy ameipokea kwa cheni ya wapokezi nyingine kupitia kwa Ibn Mas´uud, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni nzuri, khaswa kwa kuzingatia kwamba imekwishatangulia Hadiyth nyingine inayoitia nguvu ya al-Baraa´ (110).

[9] Alikuwa mwaminifu na mwanachuoni. Alikuwa anamfanyia kazi ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz Masuul.

[10] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh kwenda mpaka kwa ´Adiy bin ´Adiy.

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiy Shaybah al-Kuufiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 48
  • Imechapishwa: 18/07/2023
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy