Msalimie yule unayekutana naye

Swali: Wakati fulani mtu anapita karibu na mnaswara au myahudi au ambaye hajui hali yake. Je, ampe salamu?

Jibu: Amsalimie yule atayekutana naye. Kama ambavo amesema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya kuulizwa: “Ni Uislamu ipi bora?” Akasema:

“Kulisha chakula na kumtolea salamu unayemjua na usiyemjua.”

Isipokuwa ukijua kuwa ni myahudi, mnaswara au makafiri wengine basi usianze kuwasalimia. Lakini usipojua msalimie utayekutana naye.

Swali: Vipi akiwa na haja kwake?

Jibu: Asimtolee salamu. Amuulize hali yake, anavyoendelea na hali ya watoto wake. Asimwambie:

السلام عليكم

“Amani ya Allaah iwe juu yenu.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23465/حكم-القاء-السلام-على-من-لا-يعلم-بحالهم
  • Imechapishwa: 26/01/2024