02. Hadiyth “Hakuna yeyote atakayetawadha akatia vizuri wudhuu´ wake na kuswali Rak´ah mbili… “

227 – ´Uqbah bin ´Aamir (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

ما من أحدٍ يتوضأ فَيُحسن الوُضوء، ويُصلِّي ركعتين، يُقْبل بقَلبه ووجهه عليهما، إلا وَجَبَتْ له الجنةُ

“Hakuna yeyote atakayetawadha akatia vizuri wudhuu´ wake na kuswali Rak´ah mbili, akauelekeza moyo wake na uso wake, isipokuwa atathubutukiwa kuingia Peponi.”[1]

Ameipokea Muslim, Abu Daawuud, an-Nasaa’iy, Ibn Maajah na Ibn Khuzaymah katika ”as-Swahiyh” yake.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/210)
  • Imechapishwa: 26/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy