Msafiri wa ndege anaona jua baada ya ndege kupaa angani

Swali: Kuna bwana mmoja amenipasha khabari kwamba alikata swawm katika uwanja wa ndege wa Riyaadh. Pindi ndege ilipopaa angani akaona jua bado liko manjano halijazama.  Ni ipi hukumu ya kukata kwake swawm?

Jibu: Kinachodhihiri ni kwamba kukata kwake swawm ni sahihi kwa sababu amekata swawm kwa kutegemea kuzama kwa jua katika mji wake. Mfano wa mtu huyu ni kama ambaye amesafiri kutoka magharibi baada ya jua kuzama hadi akafika mashariki katika mji mwingine ambapo jua bado halijazama. Swawm yake ni sahihi. Kwa sababu ameenda katika mazingira mengine yasiyokuwa yake. Kukata kwake swawm hakudhuru kitu. Ni ukataji swawm sahihi na swawm yenyewe ni sahihi.

Endapo atasafiri kutoka Jeddah baada ya kuwa amekwishakata swawm na akaenda Shaam au Misri akakuta jua bado halijazama, basi swawm yake ni sahihi. Vivyo hivyo ni kama mfano wa mwenye kusafiri kutoka Tunisia baada ya kuwa jua limekwishazama hali ya kuwa amekwishafuturu ambapo akafika Algeria au Maroko na jua bado halijazama, basi swawm yake ni sahihi. Siku yake yeye imekwisha.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/3994/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%85%D9%86-%D8%A7%D9%81%D8%B7%D8%B1-%D8%A8%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B7%D8%A7%D8%B1-%D8%AB%D9%85-%D8%B1%D8%A7%D9%89-%D8%A7%D9%84%D8%B4%D9%85%D8%B3-%D8%A8%D8%A7%D9%84%D8%AC%D9%88
  • Imechapishwa: 11/05/2020