174 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

مَنْ دَعَا إِلَى هُدَىً، كَانَ لَهُ مِنَ الأَجْرِ مِثْلُ أجُورِ مَنْ تَبِعَه، لاَ يَنْقُصُ ذلِكَ مِنْ أجُورِهمْ شَيئًا، وَمَنْ دَعَا إِلَى ضَلاَلَةٍ، كَانَ عَلَيهِ مِنَ الإثْمِ مِثْلُ آثَامِ مَنْ تَبِعَهُ، لا يَنْقُصُ ذلِكَ مِنْ آثَامِهِمْ شَيئًا

“Atakayelingania katika uongofu, ana ujira mfano wa ujira wa atakayemfuata, hatopungukiwa na hilo katika ujira wa atakayemfuata na chochote. Na atakayelingania katika upotevu, basi ana madhambi mfano wa madhambi wa ambaye atakayemfuata, hatopungukiwa na hilo katika madhambi yao na chochote.”[1]

Tambua kuwa kulingania katika uongofu na madhambi kunakuwa kwa maneno kama kwa mfano aseme “Fanya kadhaa.” Vilevile inakuwa kwa matendo. Hili ni khaswa yule mtu anayeigwa na watu. Ikiwa ni mtu anayeigwa kisha akafanya jambo, ni kama vile amewaita wafanye tendo lile. Na ndio maana wengine hutumia hoja kwa anayofanya na kusema “Mbona fulani amefanya kadhaa. Hivyo inajuzu. Ameacha kadhaa. Hivyo inajuzu.”

Hapa kuna dalili inayoonesha msababisha ni kama mtendaji. Huyu ambaye amelingania katika uongofu ndio amesababisha. Kwa hiyo anapata ujira sawa na yule mtendaji. Na yule aliyelingania katika madhambi ndio amesababisha. Kwa hiyo anapata na madhambi sawa na yule mtendaji.

[1]Muslim (2674).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/361)
  • Imechapishwa: 15/01/2025