Anayeingia katika Uislamu anatakiwa afunzwe ili aingie kwa ujuzi. Kuna wanaoingia kwa kuchukulia tu kama ni dini lakini haijui. Akishawekewa wazi desturi za Kiislamu anaritadi. Kufuru yake ya pili inakuwa kubwa kuliko ile ya kwanza. Kwa sababu hakubaliwi mtu kuritadi. Aambiwe ima arudi katika Uislamu au tunakuua.

Kwa ajili hii ni wajibu juu yetu leo mbapo kumekithiri makafiri kati yetu miongoni mwa manaswara, mayahudi, washirikina na wengineo, pale tunapowalingania katika Uislamu kwanza tuanze kwa kuwabainishia ni nini Uislamu. Tuwafafanulie nao ili waweze kubainikiwa ili aweze kuingia kwa ujuzi. Haitoshi kuwaambia “Silimuni” tu. Hawajui ni yepi yanayowawajibikia juu ya haki ya Allaah katika Uislamu. Wakiingia baada ya kuujua Uislamu basi sisi tunakuwa ni wenye udhuru hapo baada pale ambapo wataritadi. Katika hali hii tutawaambia warudi katika Uislamu na la sivyo tunawaua. Ama kuwalingania kwa sura ya ujumla, huu ni ulinganizi wenye mapungufu.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/367)
  • Imechapishwa: 15/01/2025