04. Hadiyth “Ziwekeni sawa safu zenu, linganisheni mabega yenu, fanyeni wepesi kwa ndugu zenu na zibeni mapengo… ”

9 – Abu Umaamah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ziwekeni sawa safu zenu, linganisheni mabega yenu, fanyeni wepesi kwa ndugu zenu na zibeni mapengo, kwani hakika kwa shaytwaan huingia kati yenu kama watoto wadogo wa kondoo.”[1]

10 – ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Zisawazisheni safu, linganisheni mabega, zibeni mapengo, fanyeni wepesi kwa ndugu zenu na msimuachie nafasi kwa shaytwaan. Yeyote atakayeunga safu, basi Allaah atamuunga, na yeyote anayevunja safu, basi Allaah atamvunja.”[2]

11 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wekeni safu sawa katika swalah, kwani hakika kuweka safu sawa ni katika uzuri wa swalah.”[3]

12 –  Anas bin Malik (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ziwekeni safu sawa, kwani nawaona nyuma ya mgongo wangu.”

Imekuja katika tamo jengine:

”Swalah ilikimiwa ambapo na Mtume wa Allaah (Swalla Allahu ´alayhi wa sallam) akatugeukia na kusema:

“Ziwekeni safu zenu sawa na simameni karibu pamoja, kwani kwani nawaona nyuma ya mgongo wangu.”[4]

13 – Abu Muusa (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalah inapokimiwa, basi zisawazisheni safu zenu…”[5]

14 – Jaabir bin ´Abdillaah al-Answaariy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika katika utimilifu wa swalah ni kule kusawazisha safu.”[6]

[1] Imaam Ahmad  (36/597) nr. (22263).

Shaykh Shu’ayb amesema:

“Ni Swahiyh kupitia zingine.”

Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb” (1/330).

[2] Ahmad na Abu Daawuud (666). an-Nasaa´iy na Ibn Khuzaymah wamepokea sehemu yake ya mwisho. Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb” (495) na ”Swahiyh Abiy Daawuud” (620). al-Mundhiriy amesema:

”Nafasi (الفُرُجَات) ni wingi wa nafasi (فُرْجَه), nayo ni nafasi iliyo wazi kati ya watu wawili.

[3] al-Bukhaariy (689), Muslim (435) na Ibn Hibbaan (2174) kwa ukaguzi wa wa al-Albaaniy.

[4] al-Bukhaariy (687, 686) na Muslim (434).

Lafudhi yake kwa Muslim:

“Kamilisheni safu zenu…”

al-Bukhaariy (692) ameongeza:

“Mmoja wetu alikuwa akiegemeza bega lake na bega la mwenzake na mguu wake na mguu wa mwenzake.” (as-Silsilah as-Swahiyhah (31) ).

[5] Imekuja kwa Muslim (404) kwa lafudhi:

“Mnaposwali, basi simamisheni safu zenu.”

Ibn Hibbaan nr. (2167), (5/540) kwa ukaguzi wa Shu’ayb.

Ibn Khuzaymah (1584), Ahmad Abu ´Awaanah na at-Twayaalisiy.

Ni Swahiyh kwa mujibu wa Shaykh al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) katika maelezo yake ya “Swahiyh Ibn Hibbaan” (2164).

[6] Ahmad (14494), Abu Ya’laa (2168) na at-Twabaraaniy katika “al-Kabiyr” (1744), ´Abdur-Razzaaq katika “al-Muswannaf” (2425).

Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy’” (2221).

  • Muhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ujuwb Taswiyat-is-Sufuuf
  • Imechapishwa: 15/01/2025