03. Hadiyth “Zisawazisheni safu zenu, kwani hakika katika kusawazisha safu… ”

4 – Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

 “Zisawazisheni safu zenu, kwani hakika katika kusawazisha safu ni katika ukamilifu wa swalah.”[1]

5 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Naapa kwa yule Ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake ya kwamba mimi nawaona mlioko nyuma yangu kama ninavyowaona mlioko mbele yangu. Sawazisheni safu zenu, zifanyeni uzuri Rukuu´ zenu na sijda zenu.”[2]

6 – an-Nu’maan bin Bashiyr (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Naapa kwamba mtasawazisha safu zenu au Allaah atafanya nyuso zenu zitofautiane.”[3]

7 – al-Baraa´ bin ´Aazib (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akipita safu kutoka upande mmoja hadi mwingine, akipangilia vifua vyetu na mabega yetu, akisema:

“Msikhitilafiane ili nyoyo zenu zisihitilafiane.”[4]

8 – Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nyoosheni safu zenu, sogeleaneni karibu na linganisheni shingo zenu. Naapa kwa yule Ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake ya kwamba nawaona mashaytwaan wakiingia kati ya mapengo ya safu zenu kama watoto wa kondoo wadogo.”[5]

[1] al-Bukhaariy (690) na Muslim (433).

Imekuja katika tamko la Muslim:

“…kwa hakika katika kusawazisha safu ni katika ukamilifu wa swalah.”

[2] Imaam Ahmad katika ”al-Musnad” (14/8) nr. (8255). Ni Swahiyh kwa mujibu wa Shaykh Shu’ayb al-Arnaa’uut.

[3] al-Bukhaariy (685), Muslim (436), Ibn Hibbaan (2162) kwa ukaguzi wa Shaykh al-Albaaniy.

Imekuja katika tamko la Muslim:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisawazisha safu zetu kama kwamba anasawazisha mishale, mpaka alipoona kwamba tumejifunza kutoka kwake. Kisha siku moja akatoka, akasimama karibu aanze kuswali. Tahamaki akaona mtu mmoja kifua chake kikiwa kimejitokeza nje ya safu ambapo akasema: “Enyi waja wa Allaah! Mtasawazisha safu zenu au Allaah atafanya nyuso zenu zitofautiane.”

[4] Abu Daawuud (664) na an-Naasa´iy. Ni Swahiyh kwa mujibu wa Muqbil al-Waadi’iy katika ”al-Jaami´  as-Swahiyh” (2/90-95). Vivyo hivyo amefanya Shaykh al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (618).  Tamko la Ibn Hibbaan linasema ifuatavyo:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akitujilia na kupangilia mabega yetu na vifua vyetu na akisema:

“Msihitilafishe safu zenu ili nyoyo zenu zisihitilafiane…” (Ibn Hibbaan (2154))

Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.

Hadiyth hii inayo tamko la pili kwa Ibn Hibbaan linalosema:

“Msikhitilafiane ili nyoyo zenu zisihitilafiane…” (Ibn Hibbaan (2158))

Hadiyth hii inayo tamko la tatu kwa ad-Daarimiy linalosema:

“Sawazisheni safu zenu ili msikhitilafiane nyoyo zenu.”

Kama ilivyokuja katika ”Swahiyh-ul-Jaamiy” (3648).

[5] Ibn Hibbaan (2163) kwa ukaguzi wa Shaykh al-Albaaniy. Kwake imekuja:

”… na sawazisheni mabega.”

Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy. Ameipokea pia Abu Daawuud (667) na an Naasaa´iy katika ”as-Sunan al-Kubraa” (889)

Ni Swahiyh kwa mujibu wa Muqbil al-Waadi’iy katika ”al-Jaamiy’-us-Swahiyh” (2/90).

Shaykh al-Albaaniy pia ameisahihisha katika ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (621) na ”Swahiyh Sunan an-Naasaa´iy” (614).

  • Muhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ujuwb Taswiyat-is-Sufuuf
  • Imechapishwa: 15/01/2025