02. Hadiyth “Sawazisheni wala msikhitilafiane ili nyoyo zenu zisikhitilafiane”

1 – Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema:

“Sawazisheni, sawazisheni na sawazisheni! Naapa kwa yule Ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake, hakika mimi nawaona mlioko nyuma yangu kama ninavyowaona mlioko mbele yangu.”[1]

2 – Abu Mas’uud al-Badriy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akipangilia mabega yetu katika swalah na akisema:

”Sawazisheni wala msikhitilafiane ili nyoyo zenu zisikhitilafiane. Wakasogee karibu nami wenye akili timamu na ufahamu, kisha wale wanaowafuata, kisha wale wanaowafuata.”

Abu Mas’uud alisema: “Leo nyinyi ni wenye kukhitilafiana zaidi.”[2]

3 – ´Abdullaah bin Mas’uud al-Hudhaliy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wakasogee karibu nami wenye akili timamu na ufahamu, kisha wale wanaowafuata, kisha wale wanaowafuata, kisha wale wanaowafuata na jihadharini na vurugu za sokoni.”[3]

[1] an-Naasa´iy katika ”as-Sunan al-Kubraa” Hadiythi (887) na pia katika ”as-Sunan as-Sughraa”. Ni Swahiyh kwa mujibu wa Shaykh al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan an-Naasaa´iy” Hadiyth (182). Imaam an-Naasa´iy ameifanyia kichwa cha khabari Hadiyht hii katika ”as-Sunan al-Kubraa na as-Sunan as-Sughraa na akasema:

”Mara ngapi alisema  ”Sawazisheni?”

[2] Muslim (432) na Ibn Hibbaan (2169) kwa ukaguzi wa Shaykh al-Albaaniy.

[3] Muslim (432) na kutoka katika ”Kitaab-us-Swalaah” (123).

at-Tirmidhiy ameongeza kabla ya maneno yake:

“Jihadharini na vurugu za sokoni” na akasema:

”… na msikhitilafiane.”

Kama ilivyo katika ”Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (228).

  • Muhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ujuwb Taswiyat-is-Sufuuf
  • Imechapishwa: 15/01/2025