Himdi zote njema ni stahiki ya Allaah, Mola wa walimwengu wote. Mwisho mwema ni kwa wachaji Allaah. Hakuna uadui isipokuwa kwa wale waliodhulumu. Swalah na amani zimfikie yule ambaye Allaah alimtuma kuwa rehema kwa walimwengu wote, Mtume wetu Muhammad; swalah na amani ya Allaah ziwe juu yake, familia yake na Maswahabah wake wote.

Ama baada ya hayo;

Huu ni utafiti wa kawaida ambao nimekusanya ndani yake Hadiyth “Ujuwb Taswiyat-is-Sufuuf fiys-Swalaah”. Lengo ni kuwazindua waswaliji juu ya jambo hilo, kwa kusimamisha safu na kuziba mapengo. Lengo jengine ni kuhakikisha swalah zao zinakamilika wafuate Sunnah za Mtume wao (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:

“Swalini kama mlivyoniona ninaswali.”[1]

Namuomba Allaah Mkarimu, Mwenye utukufu, kwa majina Yake na sifa Zake, kwamba aifanye kuwa kwa ajili ya uso Wake Mtukufu, atujaalie mimi na ndugu zangu waumini kupata elimu yenye manufaa, matendo mema, kufaulu kwa kupata Pepo na kuokoka na Moto. Hakika Mola wangu ni Msikivu wa maombi.

Swalah na amani zimshukie Mtume wetu Muhammad, familia yake na Maswahabah zake kwa wingi.

Hudaydah – Masjid-us-Sunnah
01/01/1428
Abu Ibraahiym

[1] al-Bukhaariy kutoka kwa Maalik bin al-Huwayrith.

  • Muhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ujuwb Taswiyat-is-Sufuuf
  • Imechapishwa: 15/01/2025