Swali: Mnasema katika kisa cha ‘Abdur-Rahmaan bin ‘Awf (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba alipomwambia ndugu yake: ”Tazama mojawapo ya wake zangu”. Je, mposaji kumtazama mwanamke anayetaka kumposa ni halali?
Jibu: Ndio, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamrisha mwenye kutaka kumposa mwanamke amtazame. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Anapomposa mmoja wenu mwanamke, basi akipata uwezo wa kumtazama kitakachomvutia kumuoa, basi na afanye hivyo. Hakika hilo ni karibu zaidi kuleta mapatano baina yenu.”
Kwa hiyo kumtazama anayemposa si tatizo muda wa kuwa si wenye kukaa chemba.
Pia alikuja bwana mmoja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akimweleza kuwa amemkusudia mwanamke na anataka kumuoa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamuuliza: “Je, umemtazama?” Akasema: “Hapana.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia: “Nenda ukamtazame.”
Ameipokea Muslim katika ”as-Swahiyh” yake.
Hii inaonyesha kuwa kumtazama mwanamke kabla ya ndoa ni jambo linalopendeza na ni miongoni mwa sababu za kudumu na ustawi wa ndoa, iwapo tu hilo linafanywa bila kukaa faragha na kwa kuwepo Mharam, mama yake au mtu mwingine anayezuia kuwa peke yao.
Jaabir bin ‘Abdillaah al-Answaariy (Radhiya Allaahu ´anh) amepokea kwamba alipomposa mwanamke na akatamani kumtazama. Akasemaa kuwa alikuwa anazunguka kwenye mashamba ya mitende ya Answaar, akijificha nyuma ya mitende na akitazama ili amuone kwa namna isiyo na uzito wa Kishari´ah, mpaka alipomuona na akampenda, kisha akamposa. Kwa hivyo ikiwa ipo njia ya kumuona kwa idhini na kwa utambuzi wake, basi hakuna tatizo. Ikiwa haiwezekani hivyo, lakini akapata nafasi ya kumuona bila yeye kujua na bila kukaa naye chemba na bila kuvunja mipaka ya Shari´ah, kupitia sehemu anayoonekana bila kutengeneza fitina, basi hilo halina shida.
Swali: Je, wazazi wanapata dhambi wakimzuia mposaji kumuona msichana wao?
Jibu: Dhahiri ni kwamba hawapati dhambi. Lakini lililo bora na lenye kupendeza zaidi ni kumruhusu amtazame. Hii ni kwa sababu ni katika sababu zinazoleta mapatano baina ya wanandoa na kudumu kwa ndoa. Aidha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamuru yule bwana kwenda kumtazama. Amri yake inaonyesha kupendeza kwa wazazi kumruhusu mposaji amtazame. Hata hivyo baadhi ya watu kwa desturi zao wanaona uzito kwa hilo. Wengine wanatoa sababu ya kwamba wanachelea akimuona asimpenda, kisha akatoa maneno na watu wakaanza kumsema na hatimaye watu wakamkimbia msichana. Hivyo wana hoja na sababu zao kunako jambo hilo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1120/هل-نظر-الخاطب-لمخطوبته-جاىز
- Imechapishwa: 09/06/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1120/هل-نظر-الخاطب-لمخطوبته-جاىز
Imechapishwa: 09/06/2026
https://firqatunnajia.com/mposaji-kupewa-fursa-ya-kumuona-anayetaka-kumposa/