24 – Ametukhabarisha hayo Khaythamah bin Sulaymaan: ´Abbaas bin al-Waliyd bin Maziyd al-Bayruutwiy ametuhadithia: Muhammad bin Shu´ayb bin Swaabuur ametuhadithia: ´Abdur-Rahmaan bin Zayd bin Aslam ametuhadithia, kutoka kwa baba yake, aliyemsimulia kutoka kwa ´Atwaa’ bin Yasaar, kutoka kwa Abu Hurayrah, kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:
”Wakati Allaah alipomuumba Aadam, alipangusa juu ya mgongo wake ambapo kikaanguka kutoka katika mgongo wake kila kizazi ambacho angekiumba mpaka siku ya Qiyaamah. Kisha Akatoa ubavu miongoni mwa mbavu zake na akamuumba Hawwaa´ kwayo. Halafu akachukua ahadi na fungamano kutoka kwao:
أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ ۖ قَالُوا بَلَىٰ ۛ شَهِدْنَا ۛ أَن تَقُولُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّا كُنَّا عَنْ هَـٰذَا غَافِلِينَ
“Je, Mimi siye Mola wenu?” Wakasema: “Ndio bila shaka, tumeshuhudia [ili] msije kusema Siku ya Qiyaamah “hakika sisi tulikuwa tumeghafilika nayo haya.”
Kisha Akaufanya uso wa kila mtu kutoka katika wana wa Aadam kwa nuru yake na akamkadiria yale yote yatayomsibu katika magonjwa ya duniani. Kisha Akawadhihirisha kwa Aadam na kusema: ”Ee Aadam, hiki ni kizazi chako.” Miongoni mwao walikuwepo wenye ukoma, wenye ugonjwa wa ngozi, vipofu na magonjwa mengine. Aadam akasema: ”Ni kwa nini Umeyafanya haya juu ya kizazi changu?” Akasema: ”Ili wazishukuru neema zangu, ee Aadam.” Aadam akasema: ”Ee Mola! Ni kina nani watu hawa ambao nawaona nuru yao inang´aa?” Akasema: ”Hawa ni Mitume kutoka katika kizazi chako, ee Aadam.” Akasema: ”Ni nani huyu ambaye nuru yake inang´aa zaidi?” Akasema: ”Huyu ni Daawuud ambaye atakuwa mwishoni mwa nyumati.” Akasema: ”Ee Mola, ni muda kiasi gani Utamfanya kuishi?” Akasema: ”Miaka sitini.” Akasema: ”Ee Mola! Mimi Utanifanya kuishi kwa muda kiasi gani?” Akasema: ”Kadhaa na kadhaa, ambapo akasema: ”Ee Mola! Mzidishie miaka arobaini ili aweze kuishi miaka mia moja.” Akasema: ”Hivi kweli unalitaka hilo, ee Aadam?” Akasema: ”Ndio, ee Mola.” Akasema: ”Tunaandika na kupiga muhuri. Sisi Tunapoandika na kupiga muhuri hatubadilishi.” Akasema: ”Fanya hivo, ee Mola.” Wakati alipokuja Malaika wa kifo ili kuichukua roho yake, akasema: ”Nini unachotaka, ee Malaika wa kifo?” Akasema: ”Nataka kuichukua roho yako.” Akasema: ”Si nimebakiza katika umri wangu miaka arobaini?” Akasema: ”Je, si ulimpa mwanao Daawuud?” Akasema: ”Hapana.”
Abu Hurayrah amesema:
”Aadam akasahau na kizazi chake pia kikasahau. Aadam akakanusha na kizazi chake pia kikakanusha.”
Muhammad bin Shu´ayb amesema:
”Abul-Hafsw ´Uthmaan bin Abiyl-´Aatikah amenikhabarisha kwamba umri wa Aadam ulikuwa miaka elfu moja.”
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 50-51
- Imechapishwa: 09/06/2026
- Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy

Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 50-51
Imechapishwa: 09/06/2026
Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
https://firqatunnajia.com/09-aadam-na-malaika-wa-mauti/