25 – Ahmad bin Ibraahiym al-Baghdaadiy ametukhabarisha huko Makkah: Muhammad bin Yaziyd at-Twabariy ametuhadithia: Muhammad bin Abiy Hammaad ar-Raaziy ametuhadithia: Ibn Sulaym ametuhadithia, kutoka kwa ´Amaarah, kutoka kwa Abu Muhammad, bwana mmoja kutoka Madiynah, ambaye amesema:
”Nilimuuliza ´Umar bin al-Khattwaab kuhusu maneno Yake (Ta´ala):
وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِن بَنِي آدَمَ مِن ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ ٰ
“Na pindi Mola wako alipochukua katika wana wa Aadam kutoka migongoni mwao kizazi chao.”
Akasema: “Nilimuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama ulivyoniuliza. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Allaah (Jalla wa ´Azz) alimuumba Aadam kwa mkono Wake, akampulizia roho Yake, akamketisha, akampangusa mgongo wake kwa mkono Wake wa kuume na akatoa kizazi. Akasema: “Kizazi na kizazi chao wataingia Peponi.” Kisha akampangusa mgongo wake kwa mkono Wake wa kushoto – na mikono Yake yote miwili ni ya kulia – na akasema: “Kizazi na kizazi chao wataingia Motoni. Wayatafanya yale matendo Niyatakayo, ambapo Niwakhitimishie kutokana na matendo yao mabaya na hivyo niwaingize Motoni.”
Abu Muhammad al-Madaniy, ambaye ameisimulia Hadiyth hii kutoka kwa ´Umar, inasemekana kuwa anaitwa Muslim bin Yasaar na pia inasemekana kuwa anaitwa Nu´aym bin Rabiy´ah. Ameipokea Maalik bin Anas katika “al-Muwattwa’” kupitia kwa Zayd bin Abî Unaysah, kutoka kwa ´Abdul-Hamiyd bin ´Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Muslim bin Yasaar, kutok kwa ´Umar, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). ´Abdur-Rahiym ar-Raqqiy amepokea mfano wake kutoka kwa Zayd bin Abiy Unaysah, kutok kwa ´Abdul-Hamiyd bin ´Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Muslim bin Yasaar, kutoka kwa Nu´aym bin Rabiy´ah, kutoka kwa ´Umar, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 51-52
- Imechapishwa: 09/06/2026
- Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
25 – Ahmad bin Ibraahiym al-Baghdaadiy ametukhabarisha huko Makkah: Muhammad bin Yaziyd at-Twabariy ametuhadithia: Muhammad bin Abiy Hammaad ar-Raaziy ametuhadithia: Ibn Sulaym ametuhadithia, kutoka kwa ´Amaarah, kutoka kwa Abu Muhammad, bwana mmoja kutoka Madiynah, ambaye amesema:
”Nilimuuliza ´Umar bin al-Khattwaab kuhusu maneno Yake (Ta´ala):
وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِن بَنِي آدَمَ مِن ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ ٰ
“Na pindi Mola wako alipochukua katika wana wa Aadam kutoka migongoni mwao kizazi chao.”
Akasema: “Nilimuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama ulivyoniuliza. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Allaah (Jalla wa ´Azz) alimuumba Aadam kwa mkono Wake, akampulizia roho Yake, akamketisha, akampangusa mgongo wake kwa mkono Wake wa kuume na akatoa kizazi. Akasema: “Kizazi na kizazi chao wataingia Peponi.” Kisha akampangusa mgongo wake kwa mkono Wake wa kushoto – na mikono Yake yote miwili ni ya kulia – na akasema: “Kizazi na kizazi chao wataingia Motoni. Wayatafanya yale matendo Niyatakayo, ambapo Niwakhitimishie kutokana na matendo yao mabaya na hivyo niwaingize Motoni.”
Abu Muhammad al-Madaniy, ambaye ameisimulia Hadiyth hii kutoka kwa ´Umar, inasemekana kuwa anaitwa Muslim bin Yasaar na pia inasemekana kuwa anaitwa Nu´aym bin Rabiy´ah. Ameipokea Maalik bin Anas katika “al-Muwattwa’” kupitia kwa Zayd bin Abî Unaysah, kutoka kwa ´Abdul-Hamiyd bin ´Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Muslim bin Yasaar, kutok kwa ´Umar, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). ´Abdur-Rahiym ar-Raqqiy amepokea mfano wake kutoka kwa Zayd bin Abiy Unaysah, kutok kwa ´Abdul-Hamiyd bin ´Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Muslim bin Yasaar, kutoka kwa Nu´aym bin Rabiy´ah, kutoka kwa ´Umar, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Ishaaq bin Mandah (afk. 395)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah, uk. 51-52
Imechapishwa: 09/06/2026
Taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
https://firqatunnajia.com/10-allaah-alimuumba-aadam-kwa-mkono-wake/