Swali: Tuliswali swalah ya mkusanyiko katika msikiti, kisha imamu akasimama kwa ajili ya Rak´ah ya tano. Maamuma wakamzindua ambapo akakaa na kutoa salamu bila kusujudu sijda ya kusahau na waswaliji wakamaliza swalah katika hali hiyo.
Jibu: Hili ni kosa. Mtu akisimama katika Rak´ah ya tano katika Dhuhr, ´Aswr au ´Ishaa’, kisha akatanabahishwa kwamba hiyo ni ya ziada kisha akarudi, basi inamlazimu kufanya sujuud ya kusahau kabla hajatoka salamu. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akizidisha au akipunguza katika swalah, hufanya sujuud mbili. Wanazuoni wametaja kuwa mtu akifanya kitendo kinachobatilisha swalah kwa makusudi, basi inampasa kufanya sujuud ya kusahau. Hakuna shaka kwamba kusimama kwa Rak´ah ya tano kwa makusudi kunabatilisha swalah. Kwa hivyo akilifanya kwa kusahau, basi inamlazimu kurudi, kukaa, kusoma Tahiyyaat, kisha kufanya sujuud ya kusahau kabla ya kutoa salamu. Akichelewesha na kufanya baada ya salamu, basi hapana shida. Ama kuacha sujuud hiyo, hilo si sahihi. Huenda aliiacha kwa kusahau na hakutanabahishwa. Lakini wajibu kwake katika mfano huu ni kufanya sujuud ya kusahau. Vivyo hivyo katika Maghrib akisimama kwenda ya nne au katika Fajr akisimama kwenda ya tatu, kisha akatanabahishwa au akakumbuka na akarudi, basi inamlazimu pia sujuud ya kusahau ili kurekebisha swalah yake.
Swali: Ikiwa alikaa katika Rak´ah ya tatu badala ya Rak´ah ya nne, kisha akatanabahishwa?
Jibu: Anapaswa kusujudu sijda ya kusahau, kwa sababu alipokaa katika Rak´ah ya tatu, alikuwa amenuia kuacha Rak´ah moja. Akitanabahishwa, basi afanye sujuud. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia yule aliyoshikwa na shaka katika swalah yake:
“Je, ni tatu au nne?” Akasema: ”Aifanye kuwa tatu, kisha aikamilishe swalah, kisha afanye sujuud ya kusahau.”
Ikiwa ataswali tano, hizo sujuud mbili zitamfanya swalah yake ikubaliwe; na ikiwa ataswali nne, itakuwa ni kumkandamiza shaytwaan.
Swali: Ikiwa akatanabahishwa baada ya kutoka msikitini?
Jibu: Arudi na afanye sujuud na wale waliopo pale.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1115/حكم-من-سها-في-الصلاة-ولم-يسجد-للسهو
- Imechapishwa: 09/06/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1115/حكم-من-سها-في-الصلاة-ولم-يسجد-للسهو
Imechapishwa: 09/06/2026
https://firqatunnajia.com/imamu-amesahau-ndani-ya-swalah-na-hakuleta-sijda-ya-kusahau/