Mnyama wa Udhhiyah amezaa kabla ya kumchinja

Swali: Nilimnunua kondoo ili nimchinje lakini akazaa kabla ya kumchinja kwa muda mchache. Nimfanye nini yule mtoto wake mchanga?

Jibu: Mnyama wa Udhhiyah anawajibika kwa kule kumnunua kwa nia ya kwamba huyu ni wa Udhhiyah au kumlengesha. Akishalengeshwa ambapo akazaa kabla ya wakati wa kuchinjwa kwake, basi atachinjwa na mtoto ni mwenye kuambatana naye.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdullaah al-Ghudayyaan

´Abdullaah bin Qu´uud

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (1734)
  • Imechapishwa: 25/07/2020