Kuzidisha katika Adhkaar za baada ya swalah

Swali: Ni ipi hukumu ya kuzidisha katika kusema “Subhaan Allaah” na mfano wake katika Adhkaar za baada ya swalah?

Jibu: Inajuzu. Lakini asinuie kwamba ni miongoni mwa zile Tasbiyh zilizofungamanishwa, bali kwamba ni Tasbiyh zilizoachiwa na kwamba analipwa thawabu ya Tasbiyh zilizoachiwa.

Swali: Akichelea kufikiri kwamba ziada hiyo ni Sunnah safi na kwamba imesuniwa kuleta Dhikr kwa sauti ya juu baada ya kumaliza swalah?

Jibu: Akichelea hivo basi asizidishe.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanz-uth-Thamiyn, uk. 35
  • Imechapishwa: 25/07/2020