Mlinganizi Awalinganie Tawhiyd Washirikina Moja Kwa Moja Au Aende Nao Hatua Kwa Hatua?

Swali: Wale wanaoyaabudu makaburi na wanawataka uokozi majini wana shirki ambazo ziko wazi. Mfano wa watu hawa mtu akiwaendea aanze kuwalingania katika “hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah” ambayo ndio Tawhiyd au aende nao hatua kwa hatua ili awaeleweshe baada ya muda mfupi kidogo?

Jibu: Aanze nao Tawhiyd. Matendo yao hayatowafaa kitu isipokuwa baada ya Tawhiyd.

Swali: Kuna ambao wanasema kuwa sisi tunawakimbiza watu kwa haya?

Jibu: Huu ni ujinga wao. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alianza kwa Tawhiyd kabla ya kuanza na swalah, zakaah wala kutoa swadaqah. Bali alianza kwa kulingania katika “hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah”.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 138-139
  • Imechapishwa: 22/01/2017