Swali: Hanaabilah (Rahimahumu Allaah) wanaona kuwa mkojo wa wanyama wanaoliwa ni msafi. Je, maoni haya ndio yenye nguvu katika masuala haya?

Jibu: Ndio. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaamrisha wanamme kutoka katika kabila la ´Uraynah kula mkojo wa ngamia. Kama ungelikuwa najisi basi asingewaamrisha kuunywa kutokamana na homa. Ikajulisha hiyo kwamba mkojo wa wale wanyama wanaoliwa ni msafi. Isitoshe ameruhusu mtu kuswali katika zizi la ngamia, pamoja na kwamba hukojoa maeneo hapo. Huu ndio msingi katika masuala hayo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (27)
  • Imechapishwa: 22/04/2021