Mke kaolewa na mume wa pili ilihali mume wa kwanza bado yupo

Swali: Kuna mwanamke alienda mahakamani kuomba talaka kuachana na mume wake, wakamuuliza yuko wapi mume wako, akasema hayupo na wala sijui alipo. Mahakama wakawa wamemuomba alete mashahidi wawili wathibitishe hilo. Mashahidi hao wawili wakathibitisha ya kwamba bwana huyo hayupo na kwamba hawajui alipokwenda. Lakini wao [mahakamani] wanajua kuwa yupo katika mji huo na anafanya kazi, na ni wenye uhakika mkubwa kwa hilo. Mahakama wakawa wamempa talaka. Baada ya hapo, akaolewa huyu mwanamke na mume wa pili na mume wa pili anajua maudhui hii kuanzia mwanzoni. Ipi hukumu ya mashahidi wawili, mwanamke huyu na mume wa pili?

Ibn Baaz: Kesi hii wairudishe kwenye mahakama ambapo walihukumu, wawarejelee na wawabainishie hali ya sasa na mahakama iangalie hukumu yake. Masuala haya yanahusiana na mahakama, mahakama ibainishiwe hali ilivyo na kwamba mume yupo, walidanganya wakati walisema kuwa hayupo. Kwa vyovyote, kesi hii ipelekwe kwenye mahakama iliyohukumu mpaka waweze kutazama hukumu yake.

Muulizaji: Shaykh, vipi kuhusu madhambi?

Ibn Baaz: Mashahidi ikiwa walidanganya [kwa kujua], wako juu yao na madhambi, pamoja na manamke huyo.

Muulizaji: Vipi na mume huyu wapili ambaye anajua hali ilivyo?

Ibn Baaz: Na huyu pia ana madhambi. Na wala haijuzu kwake kumuoa naye anajua kuwa mume wake bado yupo, akamchukulia haki yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarallsubjects&schid=8177
  • Imechapishwa: 31/01/2024